patanisho.reloaded

PATANISHO: Baada Ya Kuzaa Watoto Watano Bwanangu Alioa Mke Mwingine Na Kututenga

Chris alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Florence akidai kuwa wawili hao hawazungumzi.

PATANISHO: Bwanangu Alidanganywa Kuwa Natongozwa Na Wanaume Kanisani

“Mimi na Florence tumeishi naye kwa miaka ishirini na tuna watoto watano. Tuko pamoja lakini hatuzungumzi vizuri.

Sasa nilikaa miezi sita bila kwenda nyumbani na wakati nilipoenda nilipata tu kuna mambo mengi na kumuuliza yeye hazungumzi. Baada ya kupiga kura nikapata kazi kiasi na nikatuma nyumbani, lakini bado nikizungumza naye hataki maneno yangu.

Isitoshe mamake alinieleza kuwa aliskia akizungumza na ndugu zake akidai kuwa ana mipango ya kusafiri hadi Nairobi.” Alieleza Chris ambaye amekuwa akiishi Kakamega huku mkewe akiwa Kisumu.

PATANISHO: Jamaa Alikuja Na Kisu Akitaka Kumuua Mama Yangu

“Yeye ndiye ana makosa na mimi, baada ya kuzaa na yeye watoto tano ameoa bibi mwingine na wamezaa mtoto mmoja. Ametusahau na sasa anashughulikia tu yule mtoto. Sasa kuna siku alileta yule mwanamke nyumbani na akanipiga na kunikata.” Alieleza bi Florence.

Photo Credits: victor TKO imboto

Read More:

Comments

comments