Gidi patanisho

PATANISHO: Baba alibomoa nyumba yangu na kupeleka mabati kwa chifu

Katika kitengo cha leo cha Patanisho, bwana David ndiye aliyeomba apatanishwe na babake bwana Joram akisema kuwa haelewi kilichotokea baina yao.

David alisimulia,

PATANISHO: Nakupenda kuliko avocados! Tusipatie shetani nafasi

Mimi mamangu alikuwa na urafiki na babangu na wakati wa kwenda nyumbani hakunikubalia kwenda kwa boma la baba. Nilipoenda nikamweleza baba anipe mahali nijenge boma.

Nikamwacha mke wangu nyumbani kwa boma nililojenga la matope na baada ya wiki mbili nikaskia baba alimwambia mke wangu kuwa atampatia nauli ili ende nyumbani kwao.”

David anasema alishangazwa na yale na isitoshe babake alibomoa nyumba yake saa kumi na mbili ya usiku na kumwambia kuwa mabati yake yalipelekwa kwa naibu wa chifu ili aendee humo.

Baada ya mzee Joram kukata simu yetu, David alifunguka akisema,

Ruto amtumia Kalonzo ujumbe kuunda muungano wa kisiasa

Labda mama wa kambo ndiye anayemshurutisha mzee anifukuze akidhani kuwa nataka kumrudisha mamangu kwa boma. Mimi nia yangu ni kujenga kwa boma ili tuishi na mke wangu.”

Bwana huyu anasema kuwa hajui kama mamake na babake walikuwa na uhusiano au walioana ki rasmi na hawezi uliza. Yeye alichokitaka ni kumjua babake ili aendelee na maisha na sasa amejipata akiyumbayumba asijue la kufanya.

Je ni mawaidha yepi unayoweza mpa bwana David?

Duale apinga matokeo ya sensa eneo la Kaskazini, ataka server zifunguliwe!

Photo Credits: Amon mwanjala

Read More:

Comments

comments