PATANISHO: Baba Yangu Alitenga Familia Yetu Mama Yetu Alipoaga

Onderi alituma ujumbe akiomba apatanishwe na babake, bwana Henry baada ya kukiri kuwa wawili hao hawana uhusiano mwema.

"Kwetu tuna nyumba mbili na mimi niko kwa nyumba ndogo. Uhusiano wetu mbaya ulianza nikiwa mdogo kwani ukilinganisha na watoto wa nyumba kubwa hakuwa anatushughulikia, hata karo hakuwa anashughulika.

Mamangu naye alianza kugonjeka na akatuaga na papo hapo babangu akabomoa nyumba ya mama yetu na kuchukua kila kitu. Isitoshe alitunyang'anya shamba letu na hadi sahii hatuna mahala pa kulima." Alijieleza Onderi.

Baadaye nilipoona ndugu yangu mkuu hashuguliki nikamuuliza baba sababu ya kufanya yale na akadai kuwa hiyo mali yote walishirikiana na mamangu na kuwa sina haki ya kudai. Aliongeza Onderi mwenye umri wa miaka 26.

Alipopigiwa simu, alikasirishwa na hatua ya Onderi kupeperusha masaibu yake redioni.

"Wewe umewahi nipigia nikakataa kuchukua simu? Ni nani anayefaa kupigia mwingine simu? Unajua mimi ni mzazi wako kweli?." Aliuliza bwana Henry huku akiwa na hasira kuu.

"Mimi sina shaka na yeye kama anadhani kuna shida yoyote anaweza tembea ili tuzungumze naye, anaweza kuja nyumbani. Shida kuu ni ana uwongo kwani kuna wakti aliniambia atanitumia fedha nimfanyie kazi fulani lakini hakufanya hilo, na hapo nikaamua nitulie. Sijamtenga hata kiasi na sina shida yoyote naye." Alijitetea baba Henry.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be