PATANISHO: Babe mahali popote uko please rudi nyumbani

Bwana Eric aliomba apatanishwe na mkewe bi Maryline, akisema kuwa alitoka usiku baada ya wawili hao kugombana naye kumtusi. Aliongeza akisema kuwa mkewe aliondoka na mtoto mmoja na kumuachia mtoto mmoja.

"Mke wangu tulikosana Sunday na hatukupigana lakini nilimtusi kabla ya kwenda kanisani. Alinikasirisha baada ya kupata kama amefua soksi na nikakosa za kuvaa, hapo nikakasirika na nikamtusi. Hapo jana ndio aliondoka na kubeba mtoto mmoja." Alisema Eric akidai kuwa mkewe ana kichwa ngumu.

"Unajua nilioa girlfriend yangu so sijui kama ni ile mazoeano, nilipata kuwa ameacha funguo za nyumba baada ya kubeba mtoto na begi yake. Nampenda sana na anajua kuwa siwezi ishi na mwingine." Aliongeza akisema wawili hao wameoana kwa miaka 11 na sasa hajui aliko.

Juhudi za kumfikia Maryline hazikufua dafu na ilibidi Eric amtumie ujumbe hewani.

Babe mahali popote uko please rudi nyumbani mtoto anakuhitaji anauliza Nicole ako wapi siwezi make it bila wewe, wewe ndio mke wangu na sina mwingine.

Mara ya mwishi nipatie tu chance ya mwisho, naomba msamaha mimi ni binadamu tu.