patanisho.kali

PATANISHO: Baby You Are Fighting With Jesus To Control My Heart

Ken Kuova kutoka Kayole aliomba apatanishwe na mkewe Rose Njeri ambaye alitoka nyumbani tarehe ishirini na nane mwezi wa nne, mwaka huu na kuelekea kwao, siku ambayo baba, Joshua Raila Odinga alipewa idhini ya kuwania urais na IEBC na kutembelea maeneo ya Jacaranda.

Alipopigiwa simu bwana Ken alieleza kuwa alikuwa kazini baada ya kumuacha nyumbani bila shida yoyote. Aliporudi nyumbani mida ya mchana hakumpata na alikuwa ameelekea nyumbani.

“Nilimpigia mamake simu na akanieleza kuwa mwanadada wake ni mgonjwa lakini nilipotaka kujua zaidi hakunieleza. Baadaye ndipo alisema kuwa naskiza mambo ya watu, namuite kahaba ambayo sio ukweli hata kidogo kwani hata kama ningekuwa na uhusiano singempigia simu kumjulia hali. Isitoshe tulikuwa tunaishi karibu na wazazi wake na ilibidi tuhame ili asiseme naskiza mambo ya watu,” alieleza Ken mwenye miaka thelathini.

Wawili hao wameoana kwa muda wa mwaka mmoja lakini bado hawajajaliwa na mtoto.

“Aliyosema ni urongo, ni ukweli kwani mahali tulihama hushinda huko, sielewi nini anafanya huko kwani tulitoka huko na kila siku lazima apitie huko, na hataki nipitie huko. Nashuku ana mpango wa kando,” alieleza ‘Shiku’ huku akiongeza kuwa kuna maneno kadhaa hajawahi mueleza, kama kuwa na bibi mwingine nyumbani.

“Kuna Shemeji fulani aliyenieleza ukweli wote akisema kuwa ana bibi nyumbani ambaye hamsaidii na hushinda akimtumania amtumie vitu, hapo nilijua ana mambo anaficha,” aliongeza Shiku.

Narudia kwa mara ya tatu, sina mke nyumbani! Alisisitiza Bwana Ken; “In fact I told you that you are competing with Jesus to control my life.”

Pata uhondo kamili kwa kusikiza hili Patanisho.

 

Photo Credits: GIDI

Read More:

Comments

comments