Patanisho: Bi Terry amfumania bwanake akila uroda na binamu yake wa kike 

Kiprono, 28, aliwasilisha tatizo linalomsumbua na kumfanya kutatizika maishani kutoka mwaka jana mwezi wa Oktoba.

Baba huyu wa watoto wawili alikosana na bibiye Terry  na akatoroka na kuenda kwao. Mzozo huu ulianza kutokota na kurindima moto kipindi bwana huyu alipoanza kumshuku kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na wateja aliokuwa anawauzia chakula katika kibanda chake.

Soma mengine hapa.

Wateja wake walikuwa mafundi wa mjengo uliokuwepo karibu na kibanda chake  na habari zilienea na kumfikia Kiprono huenda mkewe akawa anachepuka na mafundi hao. Wivu mwingi ukamwingia na akaanza kumshuku sana na kuanza kudadisi tetesi hizi ili aweze kuufahamu ukweli wa mambo.

Alifika nyumbani kwake saa mbili za usiku na kumkosa chumbani huku watoto wao wawili wakiwa katika hali ya upweke.

Hapa hakusita na akaamua kumpigia simu mkewe ili kujua aliko. Mama Derrick hakuchukua simu ila aliikata. Alikuwa na mafundi wake kwenye mjengo akiwauzia chakula na alihofia kuenda nyumbani kama amechelewa kwani bwanake angemchapa.

Kwenye laini ya simu na kituo cha Redio Jambo kipindi kinachoruka kila asubuhi patanisho alionekana mwenye masimango na kusononeka kwani alikuja kupata ulikuwa udaku wa majirani uliofanya amshuku mkewe. Hadithi hizi za udaku wa majirani zilitia shubiri ndoa yake ya miaka 5.

Baada ya kutoroka na kwenda kwao, mama Derrick alirudi anapofanyia kazi na kumfumania bwanake akila uroda na binamu yake wa kike ambaye walijuana kipindi na ambapo alikuwa anawatembelea nyumbani kwao. Kiprono aliichukua namba yake ya simu  na kuanza kumtongoza.

“Alinipata naye kwa chumba cha kukodisha na akaanza kulia. Hata hakumpiga cousin yake.”

Alipopigiwa simu na Gidi, mama Derrick alifunguka mwanzo mwisho kuhusu jinsi bwanake alisaliti penzi lao.

“Huyo alinikosea sana. Yaani ananiacha amenimalizia na kuenda kwa cousin kufanya naye sex. The same day !” alishangaa Terry.

“Si hata wewe uanweza mpatia miaka 10?” aliuliza Terry.

Akionekana kusimama kidete na msimamo wake Bi Terry alisema atarudi baada ya muda alioutaja mbeleni.

“Nishamsamehe lakini hiyo miaka 10 kwanza iishe…yaani nikapata macd kwa nyumba. Sijui alikuwa ameniwekea nikuje kuona ama?”

Kiprono alimsingizia shetani kwa majaribu ya kutoka na binamu wa Terry kimapenzi

“Gidi hiyo ni shetani tu ata mimi sikuelewa vile kitu yenyewe ilihappen mwongeleshe apunguze miaka Gidi .” aliomba Kiprono.