aaaaaaaaaa

Patanisho: Bibi amtoroka bwanake baada ya kuuza shamba

Katika Patanisho leo Peter, 41, alipiga simu katika kipindi kinachopendwa sana na kinachoruka katika kituo cha utangazaji cha Redio jambo kila siku.

Kwa njia ya kutuma ujumbe Peter alieleza  wazi wazi kuwa amekuwa katika matatizo yanayoikumba ndoa yake ya miezi 6 tangu mwaka jana.

Hawahitaji Patanisho! How Rashid Abdalla resolves disputes with wife Lulu Hassan

Ndoa yake na Caroline ilizama katika giza totoro kipindi na ambapo aliuza shamba lao. Baada ya Peter kuuza shamba, mkewe alimtaka abomoe nyumba waliokuwa wanaishi ili wayachukue mabati wakajenge nyumbani kwao.

Ili waweze kuukamilisha mjengo, wawili hawa walihamia jijini Nairobi na kukodisha chumba. Ndoa yao iliingia shubiri na wakatengana  huku Caroline akimpotelea Bwana peter.

Mtangazaji Ghost alimpigia Caroline simu ili apate kusikiliza kesi hiyo kutoka kwake. Mwanamke huyu ambaye hana mtoto na Peter alichukua simu na kunyamaza ikiashiria ghadhabu aliyo nayo kwa bwanake.

Soma mengine hapa.

Patanisho: Bi Terry amfumania bwanake akila uroda na binamu yake wa kike

Peter alionekana amechoshwa na maisha ya upweke na kutokwa na maneno mengi. Hata hivo aliyasema ya moyoni kwa mpenzi wake huku akiamini anamskiliza

“Kama nilikukosea unisamehe. Naomba msamaha turudiane tuishi kama bwana na mke.Najua ulikasirika kwa sababu nilichukua simu yako ila naomba msamaha wako.”

Ghost alijaribu kumuuliza ni kwa nini bibiye amenyamaza na Peter akaeleza kuwa hayo ni mazoea yake.

“Huwa anapokea na haongei . Naomba msamaha kwake kabisa anisamehe. Najua nilinyanganya yeye simu lakini nitamrudishia.”

Peter alikiri yeye kuwa ana macho ya nje katika mahusiano kumechangia mkewe kumkimbia

“Unajua ile tamaa ya kuwa na wanawake wengi iliniingia lakini nitaacha uasherati. Najua kuishi bila mwanamke ni kitu ngumu sana.”

Photo Credits: Courtesy

Read More:

Comments

comments