PATANISHO: Bibi yangu aliniacha baada ya mwanamke mwingine kupokea simu yangu (audio)

Colins alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe.
"Nimekaa na mke wangu kwa zaidi ya miaka tisa. Tumepitia mengi sana na huyu mke wangu na nampenda sana kwa hivyo naomba mnipatanishe. Niliitwa na rafiki yangu Nairobi kazi tukaanza kuishi naye ambapo pia alikua anaishi na dada zake.

Nikiwa huko nilikua na line ya simu amabayo sikua naitumia na niliiweka tu kwa meza ambapo huyu dada mmoja akaichukua akaanza kuitumia.

Siku moja nikiwa siko nyumbani, bibi yangu alipiga ile line na dada ya huyu rafiki yangu akaweza kuipokea na hapo ndipo mke wangu aliniacha."

Gidi na Ghost walimpigia bibi yake Collins ambaye alisema;

"Mimi nilimkataza huyo mzee asiende Nairobi lakini akaenda.

Siku moja nikampigia mamba ya Airtel, ambapo mwanamke ndiye alishika ile line.

Nikamtumia rafiki yangu aulize huyo mwanamke ni nani, huyo mwanamke alitoboa siri yote akasema yeye ni bibi ya collins na wanakaa na yeye Nairobi."

Pata uhondo kamili;