PATANISHO: Bibi yangu alinishika na mpango wa Kando

Bwana Mwadime alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe akidai mkewe ameondoka nyumbani kwa mda wa wiki mbili baada ya kumpata na mpango wa kando.
"Aliskia tu nikiongea na simu na after nimeingia kwa nyumba nikaacha simu kwa meza, nikatoka nje akachukua number akapiga ingawa yeye hakushika. Sasa tukagombana kiasi , nikamwambia kama ni kwenda siwezi kuruhusu kwenda usiku sasa nikamwambia alale kama ni kuondoka ataenda asubuhi.

Aliamka akaniwacha nimelala akajipanga na akaenda." Alieleza akisema kuwa mawasiliano yao hayajakuwa sawa kwani juzi mkewe alimtumia ujumbe akisema anataka kurudi kuchukua vitu vyake.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka minne huku mpango wa kando wamekuwa pamoja kwa miezi minane.

Alipopigiwa simu mama Agnes alisema kuwa mumewe alikuwa anazungumza na wanawake wengine wakiwa kitandani pamoja.

"Nikamuuliza na aka kana, nikamwambia number ndio hii imepigwa alipopigiwa nikashika na yule mwanamke aliposikia sauti yangu akakata simu. Kumuuliza nani huyo akakasirika na akataka kunipiga, hiyo number nikachukua na nikaweka kwa simu yangu lakini nikimpigia yule mwanadada hukata simu akiskia sauti langu." Alieleza.

Sikiza uhondo kamili.