PATANISHO: Bibi yangu huvaa longi kwa kitanda ninapotaka mahitaji yangu ya ndoa

Yule ambaye tunapatanishi hiv leo ni bwana paul ambaye alikosana na mke wake jumapili iliyopita, na walichokosania ni ulevi wa Paul.

Paul anatabia ya kulewa, na kugombanisha mkewe juu ya mambo ya kifamilia. Sasa hivi  mke wake ako kwao nyumbani na wamesiliana lakini wamekosa kusuluhisha hayo maneno.

Wamekaaa kwa ndoa miaka sita na wamefanikiwa na watoto watatu.

Paul wa miaka 30, na bi Zipporah ni wa miaka 24 hawaskizani.

Paul alikataa kufafanua na kusema mkewe apigiwe simu.

Bi Ziporrah alijibu huku akisema, 'huyo mwanaume anakunyagwa pombe ananisumbua kwa nyumba, mimi ndio nashugulikia kila kitu nyumbani. hiyo ni sababu yangu ya kuamua kutoroka nyumbani, ana tabia ya kunichomea nguo zangu na mimi ndio tegemeo nyumbani'.

'Hata shambani haendi, na hiyo pesa ya kukunyuwa anaenda kibarua ndio aweze kukunywa'.

Paul alijitetea huku akisema 'ile kidogo napata ni ya kuchangia mambo ya nyumba',

'Nakunywa pombe kwasababu bibi yangu anapokea simu usiku na nahofia mke wangu ana mpango wa kando'.

Bi Zipporah alisema Paul huwa hafanyi bidii kwa maswala ya kimapenzi, na ndo maana Ziporrah hulalal na trouser kumi ilikumzuia bwanake kufanya kimapenzi naye. Wolololo! Je Paul atawacha pombe?

Skiza kanda ifuatayo kama Paul na Zipporah watapata suluhu;