PATANISHO: Bibi Yangu Ni Mkali Huwaka Moto Ya Blue!

Kamau kutoka Ol Kalou alituma ujumbe akiomba apatanishwa na mkewe bi Naomi ambaye walikosana mwanzo wa mwaka huu, akidai kuwa amejaribu kwa hali na mali ili mkewe arudi nyumbani lakini ameshindwa.

"Nilikuwa nafanya kazi ya bodaboda na pikipiki yangu, babangu anayeishi Nyahururu akashikwa na polisi. Sasa ilibidi nimeuza pikipiki ili awachiliwe kwani alikuwa anadaiwa elfu mia moja.

Mbeleni hatukuwa na shida na mke wangu kwani nilikuwa na mali na hapo akaanza ugomvi baada ya kuona kuwa sina kazi kama hapo mwanzo. Tunapozungumza mke wangu alirudi kwao Ol Kalou na kila tunapozungumza hana dalili za kurudi nyumbani." Alijieleza Kamau akidai kuwa wawili wamekuwa kwa ndoa ya miaka miwili.

Wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja.

Alipopigiwa simu bi Naomi alikatiza mawasiliano yetu kabla ya Kamau kutupa uhondo zaidi jinsi mkewe huwa mkali kuliko pilipili.

"We! Unajua mke wangu kweli? huyo ni mkali sana huwaka moto ya blue!"

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be