PATANISHO: Bwana alichoma nguo na kunyoa dreadlocks zangu

patanisho new
patanisho new
Moses kutoka Rongai alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Gloria akidai kuwa walikosana na mkewe kwenda nyumbani na watoto.

Juhudi za Moses kurudiana na mkewe huzimwa na mama mkwe.

"Tumekuwa tukizozana kwa nyumba kidogo kidogo na sikuwa najua kuwa mama huwa anaweka mambo kwa roho kila tunaposuluhisha. Siku moja nilikuta tu amefunga virago na kuondoka na watoto.

Nikajipanga kikao na wazee kwetu nyumbani na wazee wakaamua arudi, na aliporudi akaenda kwa mamake na akapeleka watoto kwa shule ipo karibu na mamake." Alieleza Moses.

Aliongeza akidai kuwa kila anapompigia mama mkwe simu yeye hudai watatatua kesi baada ya miezi sita.

Kulingana na Moses, wawili hao walikuwa na mipango ya kando na waliwacha hizo tabia na kisha kutatua yote.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka 13 na tayari wamejaliwa watoto wawili.

Alipopigiwa simu, bi Gloria alisema kuwa familia zote zishazungumza na kuwa ana msimamo wake ambao anafaa kuheshimu.

"Ananiharakisha sana I think he needs time by himself na pia mimi what I have gone through I think we both need some time off. " Alisema Gloria.

Akizungumzia shida zilizowakumba, Gloria alisema kuwa mumewe aliwahi mchomea mavazi yake na pia kumkata nywele zake.

"What annoyed me most is that this guy burnt all my clothes and they are made up of memories and ended up shaving my dreadlocks."