gidi na ghost asubuhi

Patanisho: Bwanangu alialika mpango wa kando kumpikia nilipoenda ushago

Doh!

Ili huyu mwanadada aweze kutulia roho yake ukiskiza vile anazungumza angependa kujua ukweli au msimamo wa huyu jamaa wake ili aweze kuamua kama aendelee kukaa pale kwao ama arudi nyumbani kwao, ilibidi Gidi apige simu mara kadha.

Bi Cynthia alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mme wake ambaye ni kama amepotea Nairobi kwasababu hapigi simu anashangaa nini imefanyika.

Tangu February Lawrence amewacha mke wake huko nyumbani na haongei na yeye na inaleta shida kidogo.

“Tulikosana mwezi wa pili. Nilimwambia nataka kwenda nyumbani akaniambia kama utaenda nyumbani hakuna shida Sasa katika hizo harakati mzee wangu akaanza kufuatiliwa kwa nyumba mara SMS, anaandikiwa na SMS na wanawake anapigiwa simu na wanawake nikamuuliza shida ni nini ni venye tuu umesikia nimeenda nyumbani akasema hapana. Sasa hiyo wiki ya kwenda nyumbani nikamwomba simu yake nitumie torch kuogea. Nikachukua simu nikaenda kwa bafuni kuoga. Sasa kitu ikaniambia angalia kwa hii simu nikapata ameandikiwa message ameandikia mwanamke mwingine ati baeb utakuja kunipikia usiku wife wangu anaenda nyumbani. Sasa nikamrudishia simu yake, ata kunisindikiza akakataa. 

Sasa nikafika nyumbanihanipigii simu sasa nikashindwa shida ni nini siku tatu zikapita hanipigii simu. Nilikuwa nimeshika number ya simu ya huyo msichana, sasa nikampigia simu kumuuliza kama anajua Lawrence. Akasema hmajui.

Sasa huyo msichana akareply kwa mzee wangu akamwambia namtusi. Sasa mzee wangu akanipigia simu akaniambia kuanzia leo ujuwe wewe sio bibi yangu. Niakaambia wazazi wangu na imagine nilikuwa na mimba ya miezi mbili. Wazazi wangu wakaniambia nipigie wazazi wake na wao wakaniambia niende kwao. Babangu akapigia huyo mzee wangu simu na kumwabia anitumie fare niende kwao. Kwa hizo harakati ya kuafuta pesa, mimba ikatoka, juu huyo mshichana alikuwa ananitusi sana.

So kumalizia ni kwamba kutoka February sijamuona hajarudi nyumbani alisema nikiwa kwao hawezi kanyanga nyumbani. Ananiandikia SMs za matusi ananiambia akona bib, nisiende nikae tuu.

Cynthia wa miaka 23, na Lawrence, miaka 30 wamekaa kwa hii uhusiano kwa miaka tatu na nusu. Wako na mtoto mmoja, na mwenye anagharamia maisha ni wazazi wake.

Je, Gidi aliweza kumpata Lawrence kupitia simu? Skiza kanda ifuatayo.

 

 

 

 

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments