PATANISHO: Bwanangu Alinichomea Kila Kitu Tulipokosana

Bi Beth alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mama rafiki yake, Mama Mwangi ambaye nikama mamake mzazi.

"Mimi nilikosana na mzee wangu huko Nakuru na akanichomea kila kitu mpaka nguo zangu kwani nilikuwa fundi. Nikasafiri hadi kwa binamu yangu Nairobi na hapo ndipo nilipopatana na mama fulani ambaye aliniweka kwake kama mtoto wake." Alieleza Beth akidai kuwa alikuwa anamsaidi yule mama kuuza chang'aa.

Nikiwa pale nikapigiwa simu kuwa mzee wangu amefariki. Sasa katika ile harakati nikatengeneza urafiki na jamaa fulani na yule mama hakuwa anataka, kwani alikuwa anataka niweke urafiki na maafisa wa polisi ili wakija pale wasichukue fedha kwani nipo pale.

Hapo akakasirika na akamvuruga yule kijana akidai kuwa nitamsaidia hadi lini kwani hakuwa na kazi. Hapo nikasafiri kutoka Nairobi na punde si punde yule mama akamfukuza kijana na kumtupia nguo zangu."Aliongeza.

Tulikuwa tunafanya kazi pamoja na ikaja ikaharibika na hiyo ndio ilifanya tukosanie hadi mambo ya pesa na akaamua kunishtaki kwa chifu kuwa sijamlipa mshahara wake." Alijietetea Mama Mwangi akiongeza kuwa hana ubaya wowote na bi Beth.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be