PATANISHO: Bwanangu alinitishia maisha na kuniita kahaba

Walter aliomba apatanishwe na mkewe Anne wa miaka sita, akidai wawili hao waligombana kiasi.

"Mke wangu alisema kuwa anataka kufanya somo fulani polytechnic na nikamlipia. Juzi juzi nikapata text fulani kwa simu yake na ikaniudhi, ilikuwa ya mapenzi hivi na ilikuwa kutoka kwa jamaa ambaye ana mke." Alijieleza Walter akidai kuwa ujumbe mwenyewe ulikuwa ukisema 'Una mzee nami nina mke ningependa tushirikiane.'

Sahii nashindwa shida ni gani kwani na provide kila kitu. Juzi nilipatwa na msiba na nilipoenda mazishi nilipata mke wangu ametoweka na akabeba watoto." Aliongeza.

Anne alisema aliamua uhusiano wao uishe. "Unajua shida yako hutaki number za wanaume kwa simu yangu na hao ni wanafunzi wenzangu ambao hatuna uhusiano wowote." Alijitetea bi Anne huku akisisitiza aliitwa malaya na kutishiwa maisha na kuwa hatorudi nyuma kamwe.

Pata uhondo kamili.

&t=885s