PATANISHO: Bwanangu Alipachika Mwanadada Mimba Kisha Akaniita Tasa

Gidi.na.Ghost.000
Gidi.na.Ghost.000
Douglas alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Lilian ambaye pamoja waliishi kwa miaka mitano bila kubarikiwa na mtoto.

Wawili hawa walikosana mwezi wa Agosti mwaka uliopita na kutengana.

"Nimezaliwa pekee yangu katika familia yetu na sasa kuna pressure nyingi kutoka kwa nyumba yetu na mke wangu alikataa kunizalia." Alielezea Douglas.

Sasa nikapata mwanadada mwingine na nikampachika mimba kwani nilikuwa najaribu kama mimi ndiye niliyekuwa na shida ya uzazi na hapo nikampachika mimba. Nimekubali nilimkosea sana."

Alipopigiwa simu bi Lilian, alikiri kuwa mwanadada huyo aliyepachikwa mimba ndiye bibiye na anaishi mashambani.

"Alimpea mwanamke huyo simu akanitusi mara kadhaa kwani alipompachika mimba alianza kuniita tasa na hapo nikaamua niondoke nimngoje mungu kwani sikutaka chuki." Aieleza Lilian.

Nilienda hospitali na nikapimwa lakini nikakosa fedha za uchunguzi zaidi lakini naye Douglas alikuwa anasukumwa sana na mamake na hapo nikaamua nijiondoe. Labda wakati wangu haujafika siwezi harakisha mambo kwani mungu ndiye anayejua mipango yake." Aliongeza huku akikataa katakata kurudiana na aliyekuwa mumewe kwani hataki kudharauliwa na mama mkwe.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be