gidinaghostapril19th

Patanisho: Bwanangu Edward anatabia ya kunitumia SMS za matusi, simtaki tena asema Bi Naomi

Mambo gani haya?

Iwapo Bibi yako ni mwanadada wa kuenda na kurudi katika ndoa, unaweza kuitisha patanisho? Hili ndilo swala lililo kera Bwana Edward asubuhi huu katika kipindi cha patanisho na Gidi na Ghost Asubuhi. Wamejaribu kukaa pamoja mara tatu na akaamua kumpina kidogo akamuuliza anaunua chakula cha jioni.

Katika kipindi cha Patanisho hivi leo, Bwana Edward kutoka Muranga, alikosana na mke wake Naomi, ambaye alitoroka 2014 na akaacha mtoto wa kike. Baadaye mwaka 2016 akarudi, kuhudhuria birthdai ya mtoto.

Alienda na kuniwachia mtoto 2014, na lakini juzi 2016 baada ya miaka miwili alirudi nyumbani tena akasemani vigumu kukaa na mamangu na danangu mdogo’.

‘Niliweza kuongea na wazazi na kujaribu kusuluhisha lakini baada ya wiki moja akatoroka tena. Bibi yangu aliweza kurudi tena lakini nikaona ni vigumu kukaa na yayae ushago, na tukarudi Nairobi pahali tulitafuta nyumba tuisihi pamoja. Nilitumia sh50,000 katika juhudi za kutafuta nyumba. Nikamwomba anunue supper siku mbili tuu lakini alikataa ndio tukalala njaa’.

‘Tunapozungumuza alirudi na anakaa Kayole. Aliniarifu alishindwa kuvumilia na shida zangu. Nataka kuomba msamaha kwasabu tuliongea maneneo makali’.

‘Nataka msamaha kwanza na labda kupatanishwa baadaye’.

Ilibidi Gidi ampatie Bi Naomi wakati ndio ajibu simu, na ndio maana katika Patanisho ni kupambana hadi ya mwisho.

Bi Naomi ama Mama Steve anavyojulikana, alikubali kuongea na Gidi akisema walikosana baada ta kutumiwa SMS ya matusi.

‘Alinitumia SMS mbaya sana, nikamaliana na yeye. Anakuwanga na madharau. Ninapo washa simu, ni matusi, mtu kama huyo unaweza ongea nini na yeye?’

Naomi alikata shauri kuwachana na yeye, ‘sitaki mambo yake tena hata kidogo, mtu anayenitusi hivyo sitaki. Na siyo mara ya kwanza kunitusi’.

Skiza kanda;

 

 

Photo Credits: wire

Read More:

Comments

comments