PATANISHO: Bwanangu hanitoshelezi kitandani

Bi Felista aliomba apewe nafasi ili apatanishwe na mamake, mama Joyce akidai kuwa alimkosea sana.

Alisimulia: Ilikuwa Jumamosi hii imepita, nina mume na huwa hanitoshelezi kitandani lakini ili happen kuna kijana ambaye tumekuwa urafiki tangia nikiwa mdogo. Sasa tukapatana Saturday na nikamwambia niko kwa mamangu.

Akaja na nikafunga mlango huku tukizungumza naye. Mama akaingia na akanipata na yule kijana na akaanza fitina, nikamweleza kuwa ni rafiki yangu lakini hakuskia.

Mama akasema nitoke na nimuache yule kijana kule, hapo nikamweleza siwezi muacha na nikang'ang'ana hadi kijana akatoweka. Nilipotoka nikamtumia ujumbe nikimweleza kuwa akitulia ataniita tuzungumze. Felista aliongeza.

Felista alijitetea akisema, nilikuwa na nia ya kufanya mapenzi naye lakini sio kwa mamangu bali tulikuwa tutoke baada ya kuzungumza.

Alipopigiwa simu mama Joyce aliskiza mwanawe kwa sekunde chache kabla ya kukatiza mawasiliano.

Felista alisema kuwa mamake hamtambui mumewe kwani hajawahi tia juhudi za kwenda kumwambia kuwa yeye ndiye anaishi na mwanawe.

"Mimi sina shida lakini yeye ajilete mwenyewe tuongee kwani mimi sina shida naye. Yeye ndiye anafanya liwe jambo kuu, mimi ni counselor na naweza mamobo kama haya." Alisema Mama Joyce.

&feature=youtu.be