PATANISHO: Bwanangu ni mchungaji lakini hajawahi kunihubiria, nina hasira naye

Katika kitengo cha patanisho Bi Bilha aliomba kupatanishwa na bwanake Isaac huku akimwomba msamaha.

Nini kilichotokea? Bilha alikosana na bwanake juu ya mtoto wa Isaac, ambaye ni mtoto wa bibi wa kwanza.

Bilha, aliyezungumza kwa hasira, aliomba kupatanishwa na Isaac baada ya wawili wao kukosana mwaka uliopita.

Isaac ni mchungaji wa kanisa jesus walks ministry.

Bilha anamasaibu mengi, huku akisema Isaac alilmletea mtoto wa mama wa kambo, na utata ukaanza wakti Bilha alijaribu kurekebisha mtoto, na tangu siku hiyo wawili hawa wakakosana.

Tangu March mwaka uliopita, Bilha hajawahi ona mume wake Isaac. Wasimamizi wamemtafuta lakini ana hepa kila wakati.

Isaac alisema ni mambo mazito na hangependa kupatanishwa kupitia simu, huku Gidi akistuka juu ya matusi kati ya hawa wawili.

Isaac alisema bibi yake amemtusi na eti amepoteza network na Isaac hakufurahishwa. Isistoshe Isaac alimuarifu Gidi vipi bibi yake Bilha alikuwa anaenda kando na ndoa, na ikabidi achukuwe hatua.

Isaac alidai mpenzi wake ashamtumia kupitia simu messages 120 za matusi. Wolololo.

Skiza kanda