PATANISHO: Bwanangu Ni Mkono Glue Na Kazi Ni Kunipiga Tu

Bwana Dennis mwenye umri wa miaka 26, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Bi Sarah mwenye umri wa miaka 23 ambaye aliondoka nyumbani bila sababu na hajarudi.

"Alipigiwa simu kutoka kwao eti kuna matanga mnamo mwezi wa nane baada ya uchaguzi na tangia wakati huo hajarudi." Alieleza Dennis ambaye wameoana kwa miaka saba.

Kulingana na Bi Sarah, "Huyu mzee hajawahi saidia watu wa kwetu nyumbani, mamangu akiwa mgonjwa hawezi mtumia chochote na si eti hana fedha anazo. Juzi nyanyangu aliaga dunia na sasa kuna zile fedha tunafaa kuchanga elfu mbili na mia tano. Jamaa hakunipa hata shilingi moja lakini siku chache kadhaa alinunua ng'ombe. Ebu fikiria."

Alisimulia bi Sarah huku akifichua kuwa isitoshe alikuwa anapigwa na anateswa mara kwa mara.

Hayo maisha ambayo umenipitishia kwanza nilikupata na mke mwingine nyumba yetu na kitandani mwetu." Aliongeza.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be