pata.pata

PATANISHO: Carol akwende huko alivunja mayai ya upendo

Bi Carol aliomba apatanishwe na ‘mzee wake’ bwana Martin huku akisema kuwa ana shida tele.

PATANISHO: Bwanangu hanitoshelezi kitandani

“Tulikuwa tumeoana kwa miaka 15, mzee wangu alikuwa anaishi Mlolongo na mimi nikaamua kwenda nyumbani kwani mamake alikuwa ameaga dunia.

Kumbe alikuwa na mwanamke mwingine kule Nairobi na alikuwa na watoto watatu bila mimi kujua. Hapo nikaondoka nikimngoja anifuate ili tutatua mambo lakini hakufanya vile.

Isitoshe, niliondoka na mimba yake na sasa nimejifungua katoto ka kike.” Alisema Carol.

Carol alisema kuwa yupo tayari kurudiana na bwanake akisema kuwa yupo tayari kumtambua yule mke mwingine na kuwa wataishi kwa amani.

Alipopigiwa simu bwana Martin alisema kuwa yupo kazini na kuwa Carol alimuibia na kujifanya mjinga na kubomoa nyumba na kupeleka vitu kwao.

PATANISHO: Mume wangu huniita scare crow

Anafaa ajipange na akwende huko kwani mungu yuko. Alivunja mayai ya upendo.

Gidi wewe ni mwanaume mwenzangu, mtu ameenda kijiji kizima akilala na kila mtu ametoka kwa roho yangu kitambo na heri hata nifariki bila mke. Alisema Martin huku akisema mkewe alimuibia hadi mbuzi.

Huku akikana hayo yote, Carol alikubali kuwa alibeba kuku wote na kwenda nao Machakos.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments