PATANISHO: Emmanuel na Joan wakosania bei ya mbuzi

Emmanuel alituma ujumbe akiomba apatanishwe na dadake bi Joan, akidai kuwa walikosana mwaka jana mwezo wa kumi.

"Nikama nina talanta ya kuuza mbuzi na kuna wakati dadangu aliniita nikachukue mbuzi wake ili nimbadilishie na nilipoenda sikumpata. Nilipochukua yule mbuzi nikauza na nikanunua ya kike lakini akalalamika kuwa nilinunua ndogo na nikala fedha zote." Alisema Emmanuel.

Jambo hilo lilimkasirisha Emmanuel na juhudi za kumpigi simu hazijawahi fua dafu.

Anadai kuwa aliuza mbuzi wa dadake 2100 na aliyenunua ni 2050 ila alitumia nauli ya shilingi 150.

Alipopigiwa simu bi Joan alisema hadai kuongelea hii story na kuwa kama Emmanuel anataka msamaha atazungumza na ndugu yao na watajua jinsi ya kusuluhisha hayo.

Kwa upande wake Emmanuel anasema hajawahi peleka mkewe nyumbani kwao kwa ajili ya madharau ya dadake na hajui la kufanya.

Hata hivyo hatukuweza kuwapatanisha wawili hawa kwani Joan alisitisha mawasiliano kati yetu na Emmanuel akisisitiza kuwa hakutaka kuzungumzia swala hilo hewani.