Patanisho: Familia imenitenga nikuona kaburi tuu alia Okada

Givinalis Okada aliomba patanisho huku akikiri kuwa maisha yake yamo hatarini.

Alisema, 'Niokoe maisha. Nimeshindwa kabisa oh my god familia imenitenga kabisa, nikuona kaburi tuu.

Kisa na maana?

Okada aliendela kusimulia kupita SMS' Mnipatanishe na mke wangu Mary Anyango ambaye alizozana na mamake huko nyumbani.'

Alipopigiliwa simu, Okada alimuarifu Gidi kuwa

Nilikosea mke wanu shuguli za nyumbani.

Akieleza kwa ufupi ni kuwa, 'ilikuwa mwezi wa tatu niko Thika nilitoka nikaenda nyumbani  pamoja na mke wangu. tulikaa huko mwezi moja katika hiyo harakati mimi nikarudi home ju ya kazi nikaacha mwanamke nyumbani akaanza kusumbuana na mamangu ju sasa kuna pesa mimi nilikuwa natuma mzazi akaona pesa hazipitii mkononi mwake inapitia kwa mke wangu 

Sasa mzazi akaona kama pesa anagawa sio venye zilikuwa zinafika. Hapa wakakasirikiana nikaambia mke wangu atoke. 

Sasa mzazi alipojua hivi akaanza kumwaongelesha mambo mengi sasa mke wangu akaichukuwa vibaya hakurudi huku kwangu Thika.

Okada amesononeka sana haelewi ni nini anaweza fanya.

Gidi alitaka kujua ikiwa mzazi ni mama au baba.

Okada alisema, 'Ni mama. Ni single mother. 

Je Okada amejaribu kumshawishi mke arudi?

Nimejaribu kumwambia arudi lakini bado roho yake ilo ngumu anasema atakuja tuu lakini mimi katika hiyo hali nimeshindwa hata cha kufanya yani niko kazi lakini watu hawajui venye niko the way naona ikisonga naona kama naweza ruhusiwa niende nyumbani juu sasa nimeshindwa kabisa.

Namba ya msichana ilikuwa imezimwa lakini Gidi aliweza kumfikia mamake Mary ambaye alionekana kuhuzunika na kumshawishi msichana wake arudi kwa mumewe.

msichana anajaribu kukataa lakini naendelea kuongeea na yeye arudi. Bado wanaoendana sasa huyo mama ndio atafanya kijana wake akose bibi.

Skiza kanda uweze kujua maamuzi ya Okada na mama mkwe kuhusu ndoa na kurudiana.