patanisho new

PATANISHO: Familia ya mke wangu walinikataa ju nimesota

Amos alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Mercy. Kulingana na Amos, wawili hao walikosana na ikambidi ahamie mahala pengine baada ya kupokea cheche za matusi kutoka kwa familia ya Mercy.

Alidai kuwa kutoka Mei, wawili hao bado hawajarudiana.

“Mke wangu tulianza kukosana tangia tuoane mwaka wa 2015. Familia yake haikuwa inataka tuishi pamoja kwa sababu nikama walikuwa wanatarajia mtu aliye na mali.” Alieleza Amos.

Ndugu yake akija kwa nyumba alikuwa anazungumza akidai nikama walikuwa wanatarajia jamaa aliye na fedha, dadake naye alikuwa ananisomea mbele ya watu.

Nikapata ajali nikaumia na nikawa nje ya kazi kwa miezi miwili na nikamwambia kuwa nahitaji usaidizi.

Sasa ilibidi nitafute mwanadada mwingine amdanganye kuwa yeye ni mke wangu ili nimpime, sijui nini ilitokea na hapo Mercy akakasirika.” Aliongeza.

Mercy aliposkia ni Radio Jambo alikataa kata kata kuzungumza nasi.

Pata ujumbe kamili.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments