PATANISHO: Hata akini block sitamsahau kwani nampenda - Saphan

Saphan, 31, kutoka Utawala alituma ujumbe akidai kuwa angependa kupatanishwa na mkewe bi Eunice, 24,  na kusema kuwa shida ni kuwa siku moja alimuachilia akatembee na kurudi nyumbani akiwa amechelewa, ambalo halikufurahisha wazazi wake.

Anasema mkewe aliondoka na kwenda Kisumu ambapo sasa anaishi na dadake.

"Nampenda sana na sitaki kumuachilia hivyo. Wakati wa holiday alisema anataka kwenda kumuona dadake na badala ya kurudi siku hiyo akarudi siku iliyofuata jioni jambo ambalo halikumfurahisha babangu." Alisimulia Saphan.

Alikasirika na kuondoka na kwenda kwa dadake, sasa hivi najaribu kumpigia lakini ameni block pia kwa Whatsapp. Niko tayari kumpokea na tuishi kwa maisha yetu mazuri." Aliongeza.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka miwili na bado hawajajaliwa na watoto.

"Mwambie awe mwanaume awache mambo ya kuskiza wazazi wake, wakati nilikuwa nafukuzwa alikuwa hapo mbona alikuwa amesimama tu hapo?." Aliuliza Eunice.

Eunice aliongeza,

Mume wangu nilimwambia naondoka na nitalala kwa dadangu na babake ndiye aliniuliza kwenye niliko na kuuliza mbona nimelala nje. Isitoshe aliniambia narandaranda nje na niliporudi akaniamrisha nifunge virago niondoke."

Kwa upande wake, Saphan anasema kuwa mkewe alimrushia maneno kwa gate na kumuamrisha asimtete mbele ya wazazi wake.

"Sirudi! Nishaamua, yeye aishi maisha yake na wazazi wake!"