PATANISHO: Hata alete wanawake kumi I am going nowhere!

Faustin Homabay aliomba apatanishwe na mpenziwe bwana Rajab, akisema kuwa wawili hao wanapanga kufunga ndoa lakini shida ni kuwa wanasumbuana kwa sababu kuna marafiki zake ambao wanamtongoza.

"Nilikuwa nafanya kazi ya nyumba Homabay na huku ndio tulijuana naye mwaka wa 2018 na tukafikia kupanga kuoana. Ana rafiki wa kiume kwa jina Roy na ananisumbua na sijui anataka na mimi. " Faustin alisema.

Alipopigiwa simu bwana Rajab alikiri kuwa hamjui Faustin ila anamju kwa jina Grace.

"Huyo msichana nilimuahidi tutaoana na nikamwambia awache kuskiza maneno ya watu. Kuna marafiki ambao tuliwacha urafiki na huyu mwanadada alipata mtoto.

Hao wamama walioko karibu naye walimwambia kuwa nina mtoto na msichana fulani ila ni uwongo na nilimwambia awache kuskiza maneno ya wenyewe." Alijitetea Rajab.

Aliongeza kuwa kama Grace anahisi hatoweza kuishi naye anaweza rudi nyumbani.

Kwa upande wake, Grace ameshikilia kuwa hataenda nyumbani kamwe na atashikilia ndoa yake na haijalishi kama bwana Rajab ataleta wake kumi.