PATANISHO: Hata kama ndoa ni kuvumilia niliona nitakufa!

Onesmus, 28, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Edith, 25, ambaye walikosana mwaka uliopita, akidai hawajakuwa wakizungumza lakini mara ya mwisho kuzungumza ilikuwa katika msimu wa Krisimasi, wakati mkewe aligoma baada yake kununua nguo za mtoto mmoja.

Anasema kuwa walikosania maneno ya masomo na pia kuskiza mambo ya watu.

Wawili hao waekuwa kwa ndoa ya miaka sita na wamejaliwa watoto wawili.

"Nilimpata akiwa mwanafunzi wa chuo kikuu na nikajitolea kumsaidia lakini ilifika mahali maneno ya fedha ikawa shida na ikabidi awache masomo. Sasa katika hiyo harakati akapata mtoto mwingine na tukaelewana tuwache mtoto akuwe kwanza na aende shuleni." Alieleza Onesmus.

Alisema kuwa mamake Edith alimpigia simu na akasema kama mwanawe haendi shuleni amrudishe nyumbani.

Wakati alinichukua alisema kuwa atanilipia shule lakini ilifika wakati akaanza madharau na ikabidi niwache shule. Ni mtu anapenda pombe, wanawake na vita sasa ningefanya nini? Nilivumilia lakini nikachoka." Alieleza bi Edith huku akisema Onesmus hata hawashughulikii wanawe.

"Si wewe ulisema huwezi nipeleka Radio Jambo na sasa si umenipeleka huko? Unaonanga hao wanawake wako wakiwa wa maana, sahii ni too late." Edith alimwambia Onesmus.

Onesmus naye aliwalaumu wachawi au mashetani kwa tabia zake.