gidi.na.ghost.patanisho

PATANISHO: Hutaki kunirudia lakini nirudishie kitambulisho changu!

Bernard aliomba apatanishwe na mkewe Mercy Auma, kutoka Gem, kaunti ya Siaya, ambaye waliishi pamoja kwa miaka tisa, kutoka 2009 hadi 2018.

PATANISHO: Mtu akiniita aninunulie pombe nitamshtaki!

“Tulikosana na mke wangu mwezi wa nne last year, mimi nilikuwa nafanya biashara ya samaki na tukaanza kuishi naye na nikamleta nyumbani ambapo nilimfunza kazi ya ushonaji.

Baada ya mda akasema nimfunze biashara ya samaki na akaanza kwenda baharini, kilicholeta ubishi ni kuwa alichukua mkopo bila kuniambia.” Alisimulia bwana Bernard.

Aliongeza,

Niliporudi nyumbani nikapata amepanga virago na ameondoka, kumuuliza hakunipa sababu ya kuondoka.

Nilipopigia simu watu wa loan, tukazungumza na tukaelewana tuishi pamoja kwa heshima. Baada ya mda mchache babake Auma alisema nimruhusu asafiri ahudhurie matanga nyumbani kwao lakini alipoenda hajawahi rudi.

PATANISHO: Bwanangu alinitenga na kutorokea Thika kwa mke mwingine

Wawili hao wamejaliwa watoto wawili.

“Kitu tulikosania siwezi sema lakini tulimaliza na kama anaona Radio Jambo ndio muhimu ni sawa. Tuliongea na tukamaliza, yale alinitendea na watu wao yalinitosha.” Alisema bi Auma kabla ya kukatiza mawasiliano kati yetu.

Tumewachana, sitaki kurudiana naye na nimeendelea na maisha yangu ila sijapata bwana mwingine.” Alisisitiza Auma kabla bwana Bernard kumuomba amrudishie kitambulisho chake alichotoweka nacho.

PATANISHO? ‘I am sorry it won’t happen again,’ – Martial apologizes for cheating on fiancee

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments