PATANISHO: Huwezi niwacha? Sawa endelea kunipenda basi!

Rodgers Wafula na mkewe Maureen ambaye alitoweka nyumbani tarehe 11/5/2019 na kumuachia watoto. Anadai kuwa anajuta sana.

"Nilimnunulia simu yenye mtandao na kutokea hapa akaanza ku chat na wanaume kwa vitu havifai, nikajaribu kumuonya na ikafika mahali hadi whatsapp ana chat na wanaume live na nikimuongelesha anasema kuwa namchunga." Alieleza Rodgers.

Nikiwa naenda kazini kawaida nilikuta watoto kwa jirani naye ameondoka, nikimpigia simu anadai atarudi lakini huwa uwongo mtupu.

Wawili hao wamejaliwa watoto wawili.

"Huyo hata story zake ni nyingi sana hata siwezi taka na yeye mwenyewe anajua alivyonikosea." Alisema Maureen akisema kuwa kama angetaka kurudi angerudi kitambo.

Aliongeza Maureen akisema, Huwezi niwacha? Sawa endelea kunipenda basi! Si uliamua kuoa kwani alienda? Kwa sasa siwezi rudi mpaka mwaka wa 2030.

Isitoshe Maureen anadai kuwa alipigiwa simu na majirani wakimuambia kuwa alikuwa na mke mwingine kwa nyumba.

"Sisi tutakusamehe hatujakataa chenye twaomba ni kuwa tafuta namna uje nyumbani maneno haya yasuluhishwe kijamii." Dadake Maureen alisema.