PATANISHO: Huyo jamaa akae tu na ujinga wake!

Onesmus alituma ujumbe akiomba apatanishwe na bi Cecilia ambaye walikuwa wameoana kwa mda wa mwaka mmoja. Kulingana naye, wawili hao walitengana baada yake kugunduliwa kuwa na mpango wa kando.

"Huyu mpango wa kando alikuwa tu wa mda na tulikosana. Ni venye huyo mwanamke alikuwa ananikazia mapenzi na sasa ikanibidi nichukue mpango wa kando.

Hapo mke wangu aliondoka mwaka jana mwezi wa saba na tangia siku hiyo hajawahi jibu simu zangu." Alielezea Onesmus mwenye umri wa miaka 27.

Bi Cecilia aliingia kwa ndoa yao akiwa na mtoto mmoja tayari.

Wawili hao hawakuwa wameoana ki rasmi lakini walikuwa katika harakati ya kupanga jinsi watakavyo watembelea wazazi wao.

"Mimi siwezi kubali story zake tena. Yeye mwenyewe huwezi muamini halafu baadaye kufika kwake napata ujumbe akiambia yule mpango wa kando kuwa yeye ndiye ananilelea mtoto." Alieleza Cecilia huku akiwa mwingi wa hasira.

Hata hivyo, Onesmus alisisitiza kuwa hata kama wawili hao hawatorudiana angependa tu kusamehewa.