PATANISHO: Huyu Sio Mtu Wa Kutolea Smile! Nilikuwa Namwangalia Naskia Kutapika

Kama kuna tuzo la patanisho ya kukata na shoka zaidi hii, ya jana nayo iligonga ndipo.

Patanisho yenyewe iligeuka kuwa tenganisho kati ya mashemeji ambao walitupiana cheche za matusi huku kila mmoja akikiri mwenzake ndiye aliye na hatia.

Yote yalianza wakti bwana Dennis Okemwa aliomba apatanishwe na shemeji yake Dezina, ambaye ni bibi ya nduguye baada ya kumtusi vibaya kwa simu.

"Mimi naishi Nairobi naye ndugu yangu anaishi Nakuru kwa hivo siku moja tukasafiri kuwasalimia na tulipofika tukatoka na ndugu yangu kuzungumza na mke wangu alipobaki na shemeji wakaanza kunizungumzia huku akidai kuwa mimi nina tabia ya kuoa wanawake na kuwatupa. Kurudi nyumbani bado yule shemeji akanipigia simu akinitusi kuwa mie ni mjinga na hata nikicheza ataniroga."

Alijieleza Dennis akisema kuwa "Nahisi kuwa ndugu yangu pia amenikasirikia kwani nahisi hueleza Shemeji yangu Dezina yote tunayozungumzia.

"Mimi ashawahi nipata na mpango wa kando? Wacha ndugu yake aje ili tujue nani anasema ukweli!" Bi Dezina alimkemea bwana Okemwa huku

akiwa mwenye wingi wa hasira.

"Mimi siongei na huyu mtu kwani matusi aliyonitusi hata msamaha wake sitaki kwani isitoshe alielekea nyumbani na kukodisha shamba langu kwa mtu mwingine, aombe msamaha kwa ndugu yake ila sio mimi. Juzi tulikosana na ndugu yake na yeye ndio alikuwa anamueleza aniwache," alifichua Dezina.

"Kwenda huko huyu bibi yangu ako smart kukushinda unaringia nini?" Aliuliza Dennis kabla ya Dezina kumjibu, "Mimi ni msmart kumliko ndio maana ulikuwa unanifinyia jicho."

Wololo, pata uhondo kamili hapa.

&feature=youtu.be