PATANISHO: Jamaa akubali kuwa na uhusiano na mama pima

Anne kutoka eldoret alituma apatanishwe na mumewe Zeblon.

Kulingana anadai kuwa walikosana mwezi uliopita na akaenda nyumbani kwao lakini amerudi hivi majuzi. Alidai kuwa bado hamna amani kwa nyumbani.

"Ilianza mwezi wa tatu ambapo bwanangu alianza kubadilika na kumuuliza shida ni gani anadai ako sawa lakini ikafika mahali alikuwa anafika nyumbani, anabadilisha mavazi halafu anaenda kubwaga pombe." Alisimulia mwanadada.

Kumbe alikuwa ameshikana na mama flani wa pombe ambaye alikuwa anaenda kunywa pombe na analala huko. Kazi ya huyo mwanamke ana tabia ya kuchukua wanaume wa wenyewe kwa miezi mitatu kisha anawaacha.

Sasa ilibidi nimemshikia kisu ili nione kama atabadilisha, ametulia lakini nataka akiri kuwa amewacha tabia zake." Aliongeza bi Anne.

Ni kweli Gidi nilikuwa na uhusiano na huyo mwanamke lakini sasa kulikuwa na vile tulikuwa tumependana na ilikuwa bahati mbaya mke wangu aligundua lakini niliomba msamaha na hayo yakaisha.. Alikuwa ni msichana mdogo na nilianguka kwa mtego. Alijitetea bwana Zeblon.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be