Patanisho: Jamaa alalamika baridi imezidi baada ya kumfukuza mkewe

Jamaa kwa jina Mwangi ambaye ako na miaka 40, amelalama kuwa baridi imezidi baada ya mkewe kuondoka.

Mwangi alitafuta usaidizi kupitia Ghost na Gidi ili wampatanishe yeye na mkewe Linet, ambaye alimuacha Mwangi baada ya kumfukuza.

Linet anasema kuwa mzee wake alifika nyumbani akiwa amelewa kupindukia na katika harakati hiyo, Mwangi alimfukuza Linet.

Lakini mwanaume ni kujitetea, Mwangi alisema kuwa siku hiyo zake zilikuwa zimeshika "mlevi" na alikuwa anafanya mzaha tu lakini alishangaa Linet aliondoka na ni wiki moja sasa na Mwangi anasema hawezi vumilia baridi tena.

Linet kwa upande wake anataka babake ahusishwe katika suala hilo ili wapate suluhu lakini Mwangi hataki wazazi wake Linet waingilie jambo hilo akisema kuwa babake Linet ana mambo mengi sana.

Linet anadai Mwangi huwa na shughuli nyingi sana kiasi ya kwamba hana muda wake lakini yeye bado anampenda.

Mwangi anamuomba Linet arudi nyumbani akijitetea kuwa siku hiyo "alikuwa amechoma ndom na mt kenya" ambayo ni bangi hivyo basi hakuwa anamaanisha yale yote aliyoyasema.

Linet alikubali kupatana na mzee wake Mwangi ili wasuluhishe jambo hilo lakini Mwangi aliapa kuwa "hawezi acha kuchoma manake hizo vitu haiwezi achika."

Aidha, Mwangi alimtaka mkewe kusikiliza Patanisho ili ajifunze maneno mengi ya kinyumbani kutoka kwa kipindi hicho kinachopeperushwa na Ghost na Gidi.