PATANISHO: Jamaa Alikuja Na Kisu Akitaka Kumuua Mama Yangu

Stephen aliomba apatanishwe na mkewe Mama Vickie akidai angependa ndoa yake iokolewe.

"Tulikosana na mke wangu toka mwezi wa pili na hadi wa leo imekuwa ngumu kurudiana.

Tunapozungumza sahii yuko kwa mamake. Napenda kuongea ukweli, shida ya ndoa yangu ilitokana na mimi na sio swala la mpango wa kando ni mambo tu ya shida ya nyumba. Nilienda kwao nikaleta vurugu kwa ile hasira na nikapatana na mamake mzazi na akapiga nduru aliponiona na kisu mkononi.

Tulikosana na mke wangu kwani nilikosa fedha na tukafungiwa nyumba na hapo tukagombana na mke wangu ambaye alielekea kwao na hapo ndio nikaleta vurugu." Alieleza Stephen akidai kila anapojaribu kuzungumza na mkewe bado ana hasira.

Wawili wao wamekuwa kwa ndoa ya miaka sita na wamejuliwa na mtoto mmoja.

Alipopigiwa simu mama Vickie, "Mume wangu alianza tu madharau ndogo ndogo kwa nyumba akipata fedha kidogo anaenda kwa betting na hata hakuwa anawajibika.

Kitu ingine ni kuwa alinitoa kwetu kabla sijaingia shuleni na sasa akahisi vibaya aliposkia mamangu ananisomesha, na isitoshe kuna siku alinichapa." Alieleza Mama Vickie huku akisisitiza kuwa hakuna vile atarudiana naye.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be