patanisho kuteseka

PATANISHO: Jamaa aliniambukiza Ukimwi na sasa ananitenga

Joy, 30, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Chebukati, 36 ambaye walikosana mwezi wa Oktoba.

“Huyu mume wangu tulichukuana naye mwaka wa 2016 mwezi wa tatu na tukaskizana tuishi pamoja. Kuna kitu kimoja hatukufanya na sijui kama ni mapenzi au nini kwani tulilala naye kabla ya kupimwa.” Alieleza Joy.

Kenya Ina Mambo! Video ya Jamaa mmoja akipiga punyeto hadharani yawashangaza wanamitandao

Aliongeza,

Tulikuwa tunatembeleana naye kila wikendi na siku moja nilimshuku kwani alikuwa anazima simu akiingia kwa nyumba na alikuwa anajitetea kuwa simu haina network. Siku moja nikaamua kupimwa na nikapatikana nina ukimwi na pia yeye alipopimwa akapatikana ana ugonjwa pia.”

Joy anasema kuwa yeye alipimwa na mpenzi wake wa kitambo na walikuwa salama na Chebukati alikiri kuwa hakuwahi pimwa hali yake. Anaongeza kuwa mumewe alimuacha na hali ambayo hawezi anza kurandaranda na kuharibia watu maisha yao.

“Ni kama baada ya kumsamehe alianza kunitenga na kutoshughulikia mambo ya nyumba.”

Alipopigiwa simu bwana Chebukati alikata simu na kuzima.

Kwa upande wake Joy anasema hana marafiki na amewachwa upweke na hali yake ni ngumu kufunguka kwa yeyote na hajui la kufanya.

Je ni mawaidha yepi unayoweza mpa bi Joy?

ROGUE BLOGGER:Mwanablogu Cyprian Nyakundi akamatwa kwa hila ya kupunja shilingi Milioni 17 kutumia vitisho

Photo Credits: Amon mwanjala

Read More:

Comments

comments