PATANISHO: Jamaa Amuudhi Ghost Mulee Kwa Kutumia Ujanja Ili Apatanishwe

Ernest alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Pauline.

"Ilikuwa mwezi wa nane mwaka huu sasa mamake akamuita ili aelekee nyumbani na mamake akamwambia kuwa anafaa kuondoka kwangu kwani mimi ni maskini.

Tumeoana kwa miaka miwili na unusu na tumejaliwa na mtoto mmoja wa mwaka mmoja na miezi minane." Alisema Ernest akidai kuwa alikuwa anamshughulikia mkewe.

Alipopigiwa simu bi Pauline, alikiri kuwa Ernest sio mumewe wala ni rafiki yake na wawili hao hawajawahi ishi pamoja wala kupata mtoto pamoja.

Ilikuja kubainika kuwa jamaa alikuwa anadanganya huku Pauline akidai kuwa wawili hao wamejuana kwa miezi kadhaa tu na kuwa anampenda, lakini ataka mambo yaendeshwe polepole.

Pata uhondo kamili.