PATANISHO: Jamaa Ana Wanawake Wengi Hutumia Logarithms Kuwahesabu

Carolyne mwenye umri wa miaka 30, aliwashangaza wengi alipoomba apatanishwe na mke mwenzwa mwenye umri wa miaka 26, akikiri kuwa maisha yamekuwa magumu bila mke mwenza.

"Mimi nilioleka 2008 baada ya miaka minne nikaskia bwanangu ana mtoto nje ya ndoa na akasema kuwa hawezi muachilia mtoto wake na basi alitaka kumuoa mwanadada huyo. Tulipopatana na mwanadada huyo nilimtusi na nikampiga sana huku bwanangu akiniunga mkono. Sasa bwanangu amegeuka ameanza kunitusi na kunipiga akisema kuwa mimi ndio sababu kuu mtoto wa mke mwenza alifariki, akisema mie ndiye niliyesababisha kile kifo. Saa hizi nimefukuzwa kwangu." Alisema Carolyne akiongeza kuwa alitaka wapatanishwe na mwanadada huyo kwani ana matumaini watarudiana na bwanake katika harakati ile.

"Mwanaume ana miaka lakini sijui alikuwa anakula nini sura inaka changa na mapenzi chungu nzima. Mimi nasomea udaktari huku mkewe akiwa wakili, Sikujua ana mke.

Katika harakati ile mwanaume ule akaniomba nimzalie na nilipopata mimba nikajua ni mapacha hapo ndipo wawili wao waliponichapa na katika harakati ile nikapoteza mtoto mmoja. Niliwasamehe lakini siwezi taka kuwa mke mwenza. Jamaa huyu ana wanadada wengi sana anaweza tumia Logarithms kuwahesabu." Alisema Lucy akiwafurahisha wengi. "Halafu hujifanya amefanya udaktari hawezi kuwa mgonjwa, jamaa ana mapenzi akikuingiza box kwisha."

Huyu jamaa amekodisha karibu nami nao wasichana wana umbea mwingi kwani nina marafiki wengi wavulana na jambo hilo humkasirisha sana. Aliongeza Lucy akisema kuwa atamuita Carol na mwanaume huyo ajaribu kuwapatanisha.

Moto kama pasi.

&feature=youtu.be