PATANISHO: Jamaa kazi ni kunitesa na hadi paka hajawahi peleka kwetu

Japhet kutoka Nairobi alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Sarah.

Mke wangu ametoweka miezi minne sasa na nikimpigia anadai atakuja lakini amekuwa muongo sana.

Mke wangu alipata ujumbe kwa simu yangu lakini haukuwa wangu lakini pia nilipata ujumbe kwa simu yake ya mapenzi huku wakizungumza na jamaa fulani wapatane na hapo tukakosana.

Ujumbe aliopata ulikuwa umetumwa na jamaa fulani mfanyikazi mwenzangu akiungumza na mpenziwe.

Kumuuliza akadai kuwa aliponipata sikumwambia chochote na kwa hivyo kila mmoja ajishughulishe. Alidai Japhet ambaye amekuwa kwa ndoa kwa miaka saba.

Wawili hao wamejaliwa mtoto mmoja.

Alipopigiwa Sarah alikiri Japhet alikuwa na shida ya kukwepa majukumu ya nyumba.

"Hataki kusomesha mtoto, ukimwambia mambo ya kujenga nyumbani hataki, tumeoana miaka saba na huyu mwanaume hajui kwetu lakini anataka niishi Nairobi bila kushughulika na mambo ya nyumbani." Alieleza Sarah.

Hata haikuwa mambo ya mpango wa kando, nilitoka nyumbani na pindi tu nilipofika nyumbani majirani walinipigia kunieleza alikuwa na vituko chungu nzima huko Nairobi." Aliongeza.

&feature=youtu.be