PATANISHO: Joyce akataa kurudiana na David baada ya kumpoteza mwanao

Hapo jana waskilizaji wa Jambo walipata vituko na uhondo kabamabe wakti bwana David alipoomba apatanishwe na mkewe Joyce.

Kulingana na David, walitengana na mkewe ambaye ni mganda kwa mda wa mwezi mmoja kisa na maana; Wawili hao waliingia kwa ndoa mapema na Joyce hakupata mda wa kuponda raha jinsi alivyotaka au alivyotamani.

Baada ya Joyce kupigiwa simu, alikiri kuwa alitoweka kwao baada ya David kuumpa mimba na kukana mwanawe.

Joyce aliyejawa na majonzi alisimulia jinsi alivyompoteza mwanao tumboni na licha ya hayo yote, bwana David hakumshughulikia na isitoshe aliwatuma wanao wengine mashinani.

Licha ya bwana huyu kumbembeleza na kutishia kutoa uhai wake kama bibiye hatamrudia, Joyce hakuwa na mda wa kubadilisha uamuzi wake.

Pata uhondo kwenye kanda ifuatayo.

&feature=youtu.be