PATANISHO: Kama Kichwa Cha Nyumba Mke Wangu Afaa Kuniomba Ruhusa Kabla Ya Kununua Shamba

patanisho sp
patanisho sp
Eric mwenye umri wa miaka 32, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Angeline, 31 ambaye walikosana mwezi wa pili mwaka huu.

"Tulikosana mwaka huu lakini sio makosa kubwa sana. Mwezi wa kumi na moja mwaka uliopita mke wangu aliniambia kuwa amepata kazi mjini Eldoret na nikamruhusu, baada ya siku tatu akaniarifu kuwa amepata shamba humo humo.

Nikamueleza kuwa angenieleza akiwa huko na ningeongeza fedha kadhaa tupate shamba lingine, hapo akanikasirikia akidai kuwa nimekuwa mkali na hapo akaondoka na kuelekea kwa dadake." Alieleza Eric huku akidai wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka kumi na miwili na wamejaliwa na watoto wawili.

"Alibeba vitu za nyumba na tangia siku hiyo hatujawahi zungumza na kila mara ninampigia simu hashiki simu zangu na wazazi wake huniarifu kuwa nafaa kumtafuta mie mwenyewe."

Aliongeza akisema haoni shida kubwa kwani mkewe angefanya hima kumuomba ruhusa kwanza kabla ya kununua shamba lile.

Mkewe Eric alikataa katakata kujibu simu zetu na hapo kumuacha mumewe upweke.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be