PATANISHO: Kama unanitaka you know what to do!

Jamaa kwa jina Joseph, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe bi Anne ambaye walitengana miaka mitatu iliyopita.

"Hata hatukukosana sana ni ile kutengana kutokana na wazazi wake. Sikuwa na uwezo wa ku support familia yangu na wao walikuwa able sasa hapo ndio shida ilikuwa." Alieleza Joseph mwenye umri wa miaka 45.

Wawili hao walikuwa kwa ndoa ya miaka minane na wana watoto wawili.

Mara ya mwisho kuzungumza naye alikuwa anadai kurudi lakini bado anaogopa. Nataka tu kujua kwenye roho yake ipo na turudiane." Aliongeza Joseph akisema sasa hivi ana mali zaidi kidogo kulingana na hapo awali.

How do you do that? Etii unasemaje? Unanipeleka kwa redio mbona, ulikuwa umenioa? Aliuliza bi Jane akisisitiza kuwa hakuwa ameolewa ila walipata mtoto pamoja.

Sasa kwa sababu umeamua kuleta hii story yote kwa redio na unanitaka fanya chenye unataka kufanya. How am I supposed to know that you are serious?" Aliuliza kabla ya kukata mawasiliano.

Papo hapo, bwana Joseph pia alikatiza mawasiliano.