PATANISHO: Karibu nimuue ndugu yangu lakini damu ni nzito kuliko maji

Victor aliomba apatanishwe na nduguye mkuu bwana Moses, ambaye walikosana tangia mwaka uliopita. Isitoshe alikuwa amepanga kummaliza lakini sasa hivi anataka wawili hao wasameheane.

By the way ilifika mahali nikataka kummaliza kwani niliona nikama wanacheza na maisha yangu. Boma yetu ni ya mama tofauti ya watoto nane.

Nilitaka kukata mti ili nipate fare niende Nairobi na huyu ndugu yangu wa tumbo moja alizuia kwani ni shamba la familia na hilo ndilo lilileta shida. Alisimulia Victor.

Tumekuwa tukitishiana maisha kwani ndugu zangu walianza kunitafuta na sikuwa na lala wala kuishi na amani kwani tulianza kutusiana kwa simu." Aliongeza akidai hafurahishwi na jinsi mambo yalivyo.

Bwana Moses, 39, alipopigiwa simu alimwambia Victor abadilike kwani amekosea wengi nyumbani.

"Wewe tu nakusamehe na ukija nyumbani njoo tuseme mawili matatu lakini mimi nilikusamehe kitambo." Alieleza Moses.

Kulingana na Victor, alikuwa ameita vijana ambao walikuwa wamepanga kummaliza nduguye lakini wakati ulipofika alishawishika kubadilisha mipango kwani damu ni nzito kuliko maji.