PATANISHO: Kazi ya mume wangu ilikuwa kuniletea hasara

Mama Amos alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe baba Amos, ambaye walikosana mwezi wa tisa akisema kuwa walikosania maneno ya biashara.

Kulingana na mama Amos, yeye ana biashara ya duka ambalo anahisi mumewe alikuwa na nia ya kuliangusha kwani alikuwa anauza bidhaa kwa bei nafuu na kumletea hasara tele.

Mume wangu kama ni unga ambayo nafaa kuuza shilingi 95, yeye akija anauza shilingi 90. So mimi nikamwambia tunatafuta faida lakini yeye husema kuwa vitu havina bei ghali na hapo nikamwambia awe anashinda kwa nyumba baada ya kazi badala ya kuuza na hapo akakasirika. Alisimulia.

Anasisitiza kuwa wawili hao walizungumza mara ya mwisho mwezi wa Disemba na nikupitia ujumbe wa simu.

Alipopigiwa simu baba Amos alisita kuzungumza nasi akidai kuwa yuko kazini kabla ya kukata mawasiliano kati yetu. Juhudi zetu za kumtafuta kwa mara ya pili hazikufua dafu kwani alizima simu yake.

Mama Amos alidai kuwa amejaribu kumtafuta lakini bwanake ni kama hana shughuli naye licha yao kujaliwa mtoto pamoja.