PATANISHO: Sijui Mbona Kijana Ana Uwoga Wa Kumuendea Mkewe Nyumbani

Fred mwenye umri wa miaka 29, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe, Ruth, 23, ambaye walikosana mwezi wa Februari.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa kwa mda wa miaka minne.

"Nilikuwa nimeitiwa kazi huko Mombasa na nikawacha mke wangu kwa nyumba pamoja na cousin yangu. Jambo hilo lilimkasirisha na akaenda nyumbani kwao.

Tulikuwa tumejadiliana kuhusu hilo lakini hakufurahishwa na tukio hilo na hapo akaamua kuondoka. Nilikuwa nashughulikia kila kitu chakula, kodi na kadhalika." Alisema bwana Fred.

"Nimekuwa nikimpigia simu hadi mwezi wa sita nikimuuliza shida ni nini, na kuna wakati alinidanganya kuwa ameolewa tayari na hadi kumpa jamaa fulani aliyedai kuwa bwanake. Lakini kufanya utafiti wangu niliambiwa kuwa huo wote ulikuwa mzaha tu. "

Alipopigiwa simu babake Ruth alisema kuwa hana ubaya na Fred na alichotaka tu ni yeye asafiri hadi nyumbani.

"Nilikuambia uje nyumbani nawe ukasema ati unasafiri hadi Kisii, sasa safiri uje tumalize maneno. Unajua yeye anaogopa ogopa sijui mbona kwani uwoga unaharibu mambo." Alisema mzee Harun.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be