PATANISHO: Kila ninapokosa pesa mke wangu hunifukuza kwangu

Bwana Sammy, 30 alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe mama Mose, 27, ambaye wamekosana vibaya kwa sababu ya swala la pesa.

Sammy anadai kuwa mkewe husema yeye huenda kuomba pesa kwa wanaume wengine.

Alisema:

Jana nikiwa kazini alinipigia simu akiniambia mtoto anahitaji fedha za mtihani na nikamwambia nitaomba jamaa wa kazini ili anikopesha.

Jamaa aliniambia hana zile fedha kwa sasa na nikamwambia mke wangu. Lile halikumfurahisha mke wangu na tangia jana hajaniongelesha.

Yule jamaa aliponipa zile fedha nikampa mke wangu ili arudishe mtoto shuleni na nikamuuliza kumbe hawezi niongelesha kama sina fedha? Akanipigia simu akidai kumbe nina fedha na sitaki kumshughulikia mtoto.

Aliniambia kuwa nisirudi kwa nyumba, na kila akisema vile na nirudi yeye hutafuta makosa ili nisirudi.

Isitoshe mkewe Sammy alimtishia kuwa ataenda kutafuta fedha kwa mwanaume mwingine na alimuarifu kuwa anafaa kujua wako wanaume wawili katika maisha yake.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka saba na wamejaliwa watoto watatu.

Wewe jana ulikuwa na pesa na ukanidanganya huna pesa na nilikuona ukinunua mtura. Alisema Mama Mose huku akimlalamikia mumewe.

Mimi ni mtu wa huruma na huruma yangu ndio inaniumiza kwani mimi sio kama wanaume wengine. Alijitetea Sammy.