PATANISHO: Kila wakati wanawake ndio hujibu simu zake

Justin, 41, ndiye aliyeomba kupatanishwa na mkewe bi Margaret, 39, akidai walikosana mwezi jana kisa na maana; Mkewe alianza kushuku ana mipango ya kando.
Justin anadai kuwa yeye hufanya kazi ya mjengo na hana mipango ya kando. Isitoshe, wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka 20 na wana watoto watatu.

"Baada ya kutengana,mke wangu kwa sasa yuko Butere ambapo anafanya kazi ya salon. Yeye husema vile mimi huenda Kakamega nina mpango wa kando." Alisema Justin akisema ameokoka.

Aliongeza,

Kuna siku alinipigia simu ambayo nilikuwa nimepeleka ku charge na mtoto msichana akajibu simu akisema siko karibu na hapo mke wangu akadhani ni mpenzi wangu. Nilijaribu kumueleza lakini hakuniamini na akakimbia kuwaeleza wazazi wangu."

Bi Margaret aliyejawa na gadhabu alisema,

Huyo mwanaume amenichosha kwani ana mipango wa kando wengi sana, mimi hufanya kazi ya salon na Januari na Februari watu hawana kazi na hataki kunisaidia.

Alipoenda Kakamega hakutaka kunisaidia na nikimpigia simu wanawake ndio hujibu na kumuuliza husema simu ilikuwa ina charge, kwani simu hu charge kila siku?

Margaret aliongeza,

Wewe unajua mimi ni mtu mkubwa na bado unatembea na wanawake, hiyo kuokoka yako ni bure na unataka kujitangaza kwa Gidi na ni shauri yako.

Anasema bwana Justin anapaswa kwenda kwao nyumbani apatane na wazazi wake kwani hata hajawahi peleka kitu nyumbani na amemzalia mtoto.