PATANISHO: Licha Ya Kumpoteza Mwanao, Lydia Na David Warudiana

Uchungu wa mzazi aujuaye mzazi wahenga hawakukosea waliponena.

Hili lilibainika asubuhi ya Jumatano wakati wazazi wawili, Lydia na David, ambao wanaomboleza kifo cha mwanao walipo sameheana na kurudiana licha ya masaibu yaliyowakumba ambayo yalipelekea matukio hayo ya kutoa moyo.

Kulingana na Lydia ambaye alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe wa miaka minne, walikosana mwaka uliopita kwa madai kuwa David alikuwa na mpango wa kando.

Lydia ambaye alikuwa amejifungua siku chache kabla ya kisa hicho, alikasirishwa na matukio hayo na kwa hasira akatoka na kumwacha mwanao.

Aliongeza kuwa siku chache baadaye alipata habari kuwa David alimtupa mwanao ambaye aliokolewa na wasamaria wema, waliompeleka mtoto huyo katika makao ya watoto.

Miezi kadhaa baadaye, mtoto huyo aliaga dunia. Kisa hicho ndicho kilicho waunganisha wapenzi hawa wawili ambao waliamua kusahau yaliyopita na kuganga yajayo, kwa kusameheana na kurudiana.

Skiza kanda hii.

&feature=youtu.be