PATANISHO: licha Ya Kumwambukiza Maradhi Ya Ukimwi, Patrick Alimsamehe Mkewe

Kipendacho roho ni dawa.

Na hayo yalibainika hapo jana wakti jamaa mmoja aliomba apatanishwe na mkewe baada ya wawili hao kutengana. Chanzo cha wawili hao kutengana ni mke wake kuwa na tabia za mpango wa kando na licha ya mkewe kumuambukiza na maradhi ya ukimwi bado ana mapenzi chungu nzima kwake.

Patrick 31, aliomba apatanishwe na mkewe Ruth, 29 kwani walikosana juu ya kitu kidogo tu na hapo mkewe akatoweka. Wawili wana mtoto mmoja baada ya kuoana mwaka wa 2009.

"Huwa tunakosana at least kila mwaka sijui ni kwa nini yeye huwa ananikosea na nikijaribu kumuuliza anaona nikama nina shida naye.Tulikosania mpango wa kando kwani yeye ndiye anaenda kando ya ndoa na nikimkanya hataki kuskia. Mimi ni fundi na huwa nasafiri maeneo kadha wa kadha.

Kuna siku nilienda nyumbani nikaelezwa kuwa mke wangu sio mzuri, akanituma dukani siku moja kurudi nikampata kwa lodging na mwanaume mwingine, kumuuliza mwanaume huyo akaniambia "Ulikuwa unaskia fununu lakini tumeifanya kwa maksudi ili uone" na nikamsamehe baada ya kuniomba msamaha. Ilikuwa 2014 na bado mwanaume huyo nashuku wanapatana bado kwani ujumbe wao waonyesha. Imagine nilimuoa mwaka wa 2009 na hakuwa amenieleza kuwa ana virusi vya ukimwi kwani nilimueleza akapimwe na akapatikana ana virusi nami sina lakini mwaka wa 2014 nikapatikana nina virusi, yeye kuskia hivyo ameanza kunidharau."

Alieleza bwana Patrick huku akiwashangaza waskilizaji na pia watangazaji Gidi na Ghost.

"Mume wangu huwajibika lakini shida kuu ni kuskiza umbea wa watu, namsamehe anarudia tena. Kuna mwanaume anashuku kuwa nina uhusiano naye nikimwambia sio ukweli haskizi, kitambo tulikuwa tumekosana nikaelekea nyumbani na huko nikapata mwanaume na aliponifuata akatufumania na tangia siku hiyo jambo hilo linamuumiza roho kwani haamini tuliwachana."

Alijieleza Ruth mkewe Patrick.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be