new.pata

PATANISHO: Mama alimkosea mke wangu akitaka kujionesha yeye ndio kichwa

Siku ya Jumanne, bwana Ali kutoka Mombasa alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Mwanahamisi, waliyetengana kwa mda wa miezi kumi sasa.

PATANISHO: Bwanangu alioa mfanyi kazi wetu na hajawahi niongelesha miaka saba

 

“Kwa kweli ni sababu yake kuondoka ni kuwa hatukukosana naye ila yeye ndiye waliyekosana na mamangu. Huku ni mashambani kwenye tuko na mara nyingi utapata tunaishi na mabibi zetu na mama zetu, sasa mambo ikatokea na wawili hao hawakupatana.

Nilijaribu kuingilia kati lakini hawakuwezana na akasinyika na akaondoka. Nimejaribu kwenda kwao mara kadhaa lakini amekataa kurudi akisema ni juu ya mama.” Alielezea Ali.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka miwili na wamejaliwa na mtoto mmoja ambaye aliondoka naye.

PATANISHO: Nampenda mke wangu hadi nimemtungia wimbo

Nampenda kwa sababu ni mama wa watoto wangu na hatukuwa tumekosana naye.” Aliongeza.

Alipopigiwa simu alidhibitisha masaibu yote aliyopitia na kudai kuwa atafikiria kwanza mipango yao wawili ili wasuluhishe yanayowakumba.

Mamako akiskia tumehamia mahali kwingine tutafanya aje?” Aliuliza Mwanahamisi kwani anahofia uhusiano wake na mama mkwe utaharibu mambo hata wawili hao wakihama.

Mamangu hampendi mke wangu lakini mie nampenda, wacha nitajaribu tena kuzungumza na mjomba na mama mdogo ili tujue tutakavyo suluhisha haya maneno.” Ali alimpa mkewe dhibitisho.

PATANISHO: Nilimuuma mke wangu kifuani kwa hasira

 Skiza kanda ifuatayo.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments