Patanisho

PATANISHO: Mama Chela hayuko tayari kurudiana na Bwana Abraham

Bwana Abraham alituma ujumbe kwa Radio Jambo asubuhi ya leo October 19th, akiomba kupatanishwa na mke wake. Alimwarifu Gidi kwamba alikoroshana na bibi yake Cecilia mwaka jana, na wakawachana.

Abraham alisema, “alinipata na mpango wa kando, akakasirika. Kumbe huyo mpango wangu alikuwa bibi ya mwenyewe. Bwanake alipiga simu na bibi yangu alishika hiyo simu yake, akamwmabia mimi niwachane na huyo mpango wangu”.

“Katika harakati za kukosana, niliomba msamaha lakini kumbe wakati huo bibi yangu alikuwa ana ongea na huyo jamaa”.

“Basi kufuatia hayo, sisi tulikubaliana kubadilisha mabibi. Nilichukua bibi yake na wangu akaenda kuishi na huyu mwanaume”.

Abraham aliendelea kusimulia, huku akisema, “ baada ya mwaka, bibi yangu alirudi kwangu na mpango wa kando akarudi kwa bwanake”.

Juzi  tulikosana na nikampiga kidogo, akatoroka, na ameniwacha na mtoto wa miaka mbili”.

“Ningetaka Gidi unipatanishe na mke wangu. Nataka nipatanishwe kwasababu nimechange”.

Gidi aliweza kupigia Bi Cecilia simu, akamuelezea kwamba Bwana Abraham anaomba msamaha.

Hao wawili waliongea na hivi ndivyo Cecilia alisema yeye mwenyewe anajua alichofanya. Ni uwongo ati niko kwa huyu jamaa. mimi nilienda nyumbani kwetu”.

Abraham aliomba msamaha kwa yale yote aliyofanya; “Nimekubali makosa ni yangu, nakumomba tuu unisaidie.

Bwana Abraham hakuweza kushauriana na kubembeleza mama chela arudi nyumbani.

Skiza kanda ifuatayo uskize wakti ambapo mama chela alikataa kurudi nyumbani;

 

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments